Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii Lindi.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi.

Mtandao huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia simu za mkononi.

Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.

"Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya simu"

Nao wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel "umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani"

Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.

Kampuni ya Halotel ambayo ina mpango wa kuwafikia asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, inalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo vilikuwa havijaunganishwa na huduma ya mtandao wowote wa simu kutoka mwanzo.

Katika hatua nyingine, kampuni ya Halotel itaweka mkazo wa hali ya juu katika kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.

Ikiwa na kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, Halotel ndiyo kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450.

Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.
Wanafunzi wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa walizopewa na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtaalamu wa masuala ya mtandao wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata wakazi wa kijiji cha Namayuni.
Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea banda la kusajili laini jijini hapo.
Aidha wakazi wa kijiji hicho  ameelezea furaha yake kwa ujio wa mtandao wa Halotel unavyowasaidia na kuwafichia siri zao, kwani mwanzoni kila mtu alijua kuwa ndio wanaenda kuongea na simu na mpaka kusababisha kuaga na kwenda umbali fulani kwaajili ya kutafuta netiweki ili aweze kuwasiliana na mtu ambaye anamtafuta.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...