Watu wengi wamekuwa wakilalamika ifikapo Jumamosi wanakuwa
wamechoka kwa usiku wa jana yake yaani
ijumaa, na wengine hushindwa kufanya shughuli zao muhimu kwa ufanisi siku ya Jumatatu
sababu ya uchovu wa wikiendi, je ni siku
ipi nzuri kwa starehe?. JovagoTanzania inakupa njia sahihi za kufurahia wikiendi yako kuanzia Ijumaa
mpaka Jumapili.
1. Ijumaa
Hii ni
siku ndani ya siku za kazi, baadhi ya watu humaliza kazi zao kuanzia saa sita
mchana na ofisi nyingine hadi jioni. Je
ni muhimu kutoka siku hii? Jibu ni
inategemea na umuhimu wa siku ya kesho yake (Jumamosi) au jinsi ya mtoko
uliouandaa. Ukiangalia kwa undani zaidi
hii siku nzuri sana kwa kupunguzia uchovu wote wa wikinzima kazini, unaweza
kutoka na wafanyakazi wenzako sehemu mbali mbali za starehe, lakini pia ni siku nzuri ya kuikaribisha vyema siku ya
pili yake ambayo ni Jumamosi, hivyo unashauriwa kama unakunywa kunywa kidogo
sana, jaribu kufanya starehe ambayo haitakuchosha mwili wako mpaka ukashindwa
kuamka siku nzima ya Jumamosi au ukashindwa kurudi nyumbani kabisa.
2. Jumamosi
Jumamosi
ni siku nzuri ya kutoka kwa mapumziko lakini pia kuna baadhi ya watu huenda
kazini na kurudi mchana, jaribu kuitumia siku hii ipasavyo kwani ni siku nzuri kwa
kupunguzia uchovu wote wa jana (Ijumaa)
na wa wiki nzima. Wengi
hupendelea kwenda ufukweni mida ya mchana na jioni, na usiku kwenda sehemu za muziki
tulivu, sinema, mpira au kwenda mbali na mji kama Bagamoyo. Lakini pia kama siku ya Jumapili ni muhimu
kwako jali muda wako ifikapo usiku na aina ya starehe utakayoifanya.
3. Jumapili.
Siku
ya Jumapili itumike kwa umakini kwani huikaribisha siku ya kazi ambayo ni
Jumatatu. Unaweza kuwa ulienda mbali na mji siku ya jumamosi, basi jaribu
kurudi mapema nyumbani. Pia ni siku nzuri kwa sinema, mpira na kupiga stori
nyumbani au kutembelea ndugu na marafiki. Hakikisha siku hii haikuharibii siku
ya kazi ambayo ni Jumatatu, bali ikupe uhuru wa kurudisha nguvu zako kazini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...