Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka Songea leo Jumatano Januari 6, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam Meck Sadiki.

------------------------
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).



Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi. Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli. 

Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi kwani amesisitiza kuwa mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji.
“Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu. 
Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo. 
Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi. Nauli mbona ipo sawa tu.

    ReplyDelete
  2. Hivi hivi DMT, UDA, KAMATA, SHIRIKA LA RELI, AIR TANZANIA NA MASHIRIKA MENGI YA UMMA YAMEKUFA SABABU YA KUPENDA NAFUU GHALI NA BURE GHALI. NCHI SASA INAFATA MFUMO WA SOKO HURIA WACHENI MCHUANO WA WAFANYI BIASHARA UAMUE BEI.
    LA MSINGI ANGALIENI NAMNA YA KUBORESHA KIPATO CHA MWENYE NCHI. MNAMKAKATI GANI KATIKA HILI? VIONGOZI WAKAE CHINI NA KUFIKIRI NI JINSI GANI TUTAONDOKA HAPA TULIPO KIUCHUMI?
    KAMA HAMPANGI BEI YA VITU VINGINE VINGI TU, KWA NINI MMEKAZANIA KUPANGA BEI ZA MABASI MIJINI?

    ReplyDelete
  3. Serikali iendeshe huu mradi, kwanza mradi huu umejengwa na serikali kwa mabilioni ya shilingi kwanini apewe mtu ambaye hakuugharamia? Tunataka mradi ufanywe kama service ya kawaida wala isiwe super profit making project kama UDA wanavyofanya sasa.

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru sana kwa kuzungumza kiswali sahihi na fasaha. Tanzania ndipo cimbuko la kiswahili lakini waandishi wengi na wasemaji wengi wanatafasiri maneno ya kingereza na kuyafanya kiswahili. Mfano: "firearm" - SILAHA YA MOTO. kiswahili ni bunduki au unataja silaha yenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...