Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki
ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya
shs. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Isiyorasmi Tanzania, Masudi
Maftah kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mikopo wa CRDB
Microfinance, Everson Temu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo
Zanzibar, Nuru Mohamed na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Dauda Salmini.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo
Zanzibar, Nuru Mohamed akizungumza baada ya kupokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo
Zanzibar, Nuru Mohamed (wa pili kushoto) akipokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8, kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki
ya CRDB, Tully Mwambapa.
Picha ya Pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...