
Mkuu wa Hazina wa benki ya Exim Tanzania, George Shumbusho akifafanua jambo mbele ya wadau wa benki hiyo kuhusu huduma mpya ya ‘Preferred Banking’ iliyozinduliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma hiyo inatoa upendeleo maalum katika utoaji wa huduma za kibenki sambamba na punguzo la gharama kwenye mahitaji ya kijamii kwa wateja wakubwa na wale wa kati wa benki hiyo.

Meneja Bidhaa wa Benki ya Exim Tanzania, Aloyse Maro akifafanua jambo mbele ya wadau wa benki hiyo kuhusu huduma mpya ya ‘Preferred Banking’ iliyozinduliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Huduma hiyo inatoa upendeleo maalum katika utoaji wa huduma za kibenki sambamba na punguzo la gharama kwenye mahitaji ya kijamii kwa wateja wakubwa na wale wa kati wa benki hiyo.
BENKI ya Exim Tanzania imezindua huduma yake mpya ya ‘Preferred Banking’ inayotoa upendeleo maalum katika utoaji wa huduma zake za kibenki sambamba na punguzo la gharama kwenye mahitaji ya kijamii kwa wateja wake wakubwa na wale wa kati.
Akizungumza kwenye uzinduzi maalum wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Bidhaa wa benki hiyo, Aloyse Maro aliyataja baadhi ya mahitaji hayo ya kijamii kuwa ni yale yanayoendana na aina ya maisha ya mteja husika (lifestyle) kama vile manunuzi (shopping), burudani, safari, maladhi ya hoteli na huduma za vyakula.
“Huduma hii imebuniwa maalum kukidhi mahitaji na huduma za kifedha kwa wateja wetu wakubwa na wale wa kati. Kupitia huduma hii wateja wetu watarajie huduma nzuri kutoka kwa mameneja mahusiano tofauti waliopo kwenye matawi yetu ili waweze kufurahia upendeleo kwenye huduma zetu za kibenki pamoja na zile za mahitaji ya kijamii kulingana na ‘lifestyle’ zao ,’’ alisema.
Alisema kupitia huduma hiyo wateja watanufaika kwa kupata huduma za kibenki masaa 24 katika siku saba za wiki kupitia simu zao (smart App), nyongeza ya muda wa utoaji huduma kwenye baadhi ya matawi pamoja na ongezeko la mashine za kutolea fedha (ATM) nchi nzima.
“Kifupi tunatambua matarajio ya mabadiliko ya kihuduma yaliyopo kwa wateja wetu. Huduma hii ya ‘Preferred Banking’ itaendana na mahitaji ya jamii ya kitanzania ambayo kwa sasa ni ile ya kuhama hama, inayoingiliana na jamii za kimataifa na zaidi yenye shahuku ya kutambulika zaidi,’’ aliongeza Mkuu wa Hazina wa benki hiyo George Shumbusho.
Ujio wa huduma hiyo ni muendelezo katika ukuaji wa benki hiyo hapa nchini ambayo hivi karibuni ilizindua uuzaji wa dhamana za muda mrefu (hati fungani) ambapo hadi uuzwaji wa hati hizo unafungwa rasmi Disemba 18 mwaka jana benki hiyo ilikuwa imefanikiwa kukusanya kiasi cha sh bilioni 19.7 kutokana na mauzo ya hati hizo tofauti na makadirio ya sh. Bilioni 10 iliyokuwa imejipangia kukusanya hapo awali.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...