Timu ya kuvuta kamba ya waandishi wa habari wanaume wa chama cha waandishi wa habari Dodoma(CPC) wakionyesha umahiri wao wa kuvuta kamba katika bonaza la kuaga na kuukaribisha mwaka 2016 lilodhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya Tigo.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Hamida Ramadhani akishangilia baada ya kufanikiwa kumkamata kuku katika mchezo wa kufukuza kuku uliofanyika kwenye Bonaza hilo.
RAIS wa umoja wa vyama vya waandishi wa habari nchini, Deogratius Nsokolo amewaasa waandishi wa habari wasio na mikataba ya ajira kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii ili kujiwekea akiba zitakazokuwa na faida hapo baadae.
Akizungumza katika bonanza la kuukaribisha mwaka 2016 lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma (CPC) na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo, Nsokolo alisema asilimia 80 ya waandishi wa habari nchini hawajaajiriwa.
“Kila moja ana wajibu wa kuhakikisha anajiunga na mifuko ya hifadhi na hata kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) ili kuwe na uhakika wa matibabu pale anapougua au familia yake’”alisema Nsokolo
Alitolea mfano katika Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kigoma wameweza kila mwandishi kujiunga na Mfuko wa LAPF ambapo kiasi cha Sh. 20,000 kinapelekwa kila mwezi.
Hata hivyo alisema kwa upande wa afya, kila mwandishi anaweza kujiunga na mfuko wa Taifa ya bima ya afya kila kwa Sh. 76,800 ataweza kutibiwa yeye na kuwakatia kadi ya matibabu watu wanne.Aidha alisema UTPC inatarajia kuiwezesha Dodoma kuwa na Ofisi ya kisasa kwa ajili ya waandishi wa habari kufanya kazi zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPC, Habel Chidawali alisema changamoto kubwa ni waandishi wa habari kukosa ofisi ya kufanyia kazi kwani baadhi ya vyombo vya habari havina ofisi mkoani Dodoma.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...