
Na. Mwandishi Wetu, Liwale
Chama cha waendesha bodaboda wilayani Liwale Mkoani Lindi chatoa mikopo ya pikipiki kwa wanachama wake wapatao 62 zenye thamani ya shilingi 92,000,000.
Chama hicho kilipata mkopo wa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi 35,000.000/= kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya na kuweza kukopeshwa kwa mwanachama mmoja mmoja na kupitia umoja wao chama kiliweza kupata pikipiki 42 na kuweza kufikia ya jumla ya pikipiki 62.
Leo wamekabidhi pikipiki mbili kwa wanachama wawili zenye thamani ya shilingi 4,400,000/= na kukabidhi kwa mwanachama mmoja bati zenye thamani ya shilingi 2,000,00/= jumla ni 6,400,000/= na wameweza kufanya marejesho ya shilingi 6,325,000/=.
Chama hicho Kina miaka Sita Tangu kuanzishwa kwake Mnamo mwezi Mei mwaka 2010 kikiwa na waanzilishi 65 pia chama hicho kinatambuliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Liwale na kimepatiwa Hati ya Utambulisho Mwaka 2014.

Mgeni rasmi bwana Wilson Nyamanga aliyekuja kumwakilisha mkuu wa wilaya ya Liwale mh,Ephraim Mmbaga.

Mgeni rasmi akikabidhi pikipiki kwa mwanacha hii leo maeneo ya ofisi za chama cha bodaboda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...