Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania NEC Kailima Ramadhani akifungua Mkutano wa Tathimini  kati ya Tume na Asasi za Kiraia kuhusu Elimu ya mpiga Kura wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2015, uliofanyika katika ukumbi wa Victoria Palace jijini Mwanza.
Pamoja na kutambua kazi kubwa iliyofanywa na Asasi za kiraia kwa kuweza kutoa Elimu ya mpiga kura na kuwahamasisha wananchi wote na wale wanaoishi maeneo yasiyofikika kwaurahisi kuweza kushiriki katika zoezi la upigaji kura.

Bado kulijitokeza changamoto za uelewa kuhusu alama sahihi inayohitajika kuwekwa katika karatasi za kura. Baadhi ya wapiga kura walikuwa wanaweka alama ya V kwa mgombea wanayemtaka na kuweka alama X kwa mgombea asiyemtaka na hivyo kupelekea kura nyingi kuharibika. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Wadau mbalimbali toka Asasi za watu binafsi wamehudhuria Mkutano huu wa Tathimini  kati ya Tume na Asasi za Kiraia kuhusu Elimu ya mpiga Kura wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2015, uliofanyika katika ukumbi wa Victoria Palace jijini Mwanza.
Washiriki kwenye mkutano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...