Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na Wabunge kutoka nchini Sweden (hawapo pichani) leo jijini Da es salaam wakati wa mkutano uliofanyika Wizarani hapo, kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden. Kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya Serikali wakati wa mkutano na Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi nchini.
Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa Sweden katika ukumbi wa Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina Tanzania na Sweden.
Katika mazungumzo yake na wabunge hao ambao wamewasili nchini kwa ziara ya kikazi, Dkt. Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na inafanyakazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma stahiki kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema Serikali imejipanga kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kuiwezesha nchi kujiendesha yenyewe na kuacha kutegemea misaada ya wahisani.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA


Hongereni kwa huo mkutano. Ushauri. Mikutano kama hii mikubwa ilenge kuuza sera za reli mpya standard gauge. Uzeni vipande vipande kwa nchi tajiri. Mfano Dar Morogoro nchi mmoja. Mnaomba Marekani kama nchi iwakopeshe. Morogoro-Dodoma nchi nyingine. Mpaka kufika kote unaweza kukuta nchi nyingine zinachangia. Nafikiri reli hii ikijengwa kwa awamu na kwa kudhirikisha nchi rafiki inaweza kujengwa na ikaisha. Au toka Dar-morogoro. Ziombwe nchi za Ulaya kusaidia. Bishara itakwenda safi.
ReplyDelete