Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya msako wa kushtukiza katika kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development Ltd iliyoko Barabara ya Nyerere Dar es salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kukamata vifaa pamoja na malighafi za kutengeneza na kutoa vibao vya namba za pikipiki kinyume na sheria.

Katika msako huo uliofanyika tarehe 19 Februari 2016 katika kampuni hiyo, Maofisa wa TRA waliweza kukamata na kutaifisha vibao vyenye namba za pikipiki 2,500 na vibao 5,600 ambavyo havikuwa na namba. Pia maofisa wa TRA walikamata malighafi za rangi ya vibao katoni tatu, pamoja na mashine ya kupaka vibao rangi yenye uzito wa kilo 155.

Mashine nyingine iliyokamatwa katika msako huo ni ya kutengeneza namba za magari yenye uzito wa kilo 902 ambayo imezuiwa isihamishwe kutoka katika kampuni hiyo pamoja na kompyuta mpakato ambayo imepelekwa katika maabara ya uchunguzi TRA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taarifa za kuwepo kwa utengenezaji wa vibao vya magari kinyume na taratibu na sheria zilitolewa na msamaria mwema ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni husika Donglinh Guo, Meneja wa Kiwanda Yong Qing Cheng na Meneja wa ghala Peng Zhan walikamatwa baada ya kutokea fujo wakati wa msako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Changombe.

Kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development LTd ndio waingizaji pekee wa pikipiki za Falcon tangu mwaka 2008 ambapo inatuhumiwa kutoa vibao vya namba za pikipiki kwa wateja wake kwa shilingi 5,000 kinyume na sheria.
Uchunguzi wa thamani ya kodi iliyopotea bado unaendelea.

Vibao vya magari na pikipiki hutolewa na kampuni ambazo zinatambuliwa na TRA baada ya kupewa idhini. Kampuni hizo ni Masasi Sign, Auto Zone, Sign Industry, Kiboko, Budda Auto works, Parkinson Ltd na Next Telecom.

Ili kujiridhisha kuwa kadi za pikipiki zinazotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ni halali, TRA ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa kadi hizo zinatolewa kihalali.

TRA inawatahadharisha wananchi kufuata taratibu na sheria ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea endapo watagundulika kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kitaeleweka tu. Hakuna kurudi nyuma. Ila taarifa nyingine zichunguzwe kabla ya kuvamia maana hila inaweza kutumika ili kuchafuana kibiashara. Inabidi kuwa makini.

    ReplyDelete
  2. Kama watanzania wengi na serikali yao wanavyoamini kuwa serikali ya watu wa China na raia wao ni watu rafiki na Tanzania inawezekana ikawa hivyo inavyoaminika lakini wachina ni watu wa kuchungwa sana kwani ni watu hatari sana katika kujihusisha na vitendo vya ufisadi. Kuna wachina wa kawaida ambao ni watu wazuri kimaana yakwamba si watu ambao wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na kuna kundi jengine la watu wa China ambalo ni muaganiko wa mtandao wa kihalifu ujikanalo kama ( Chinese Mafia) wengi wao ni wale tunawaona wakija katika nchi zetu bila yakuwa na kazi maalum za kufanya ukweli ni kwamba wachina wa namna hiyo wana kazi zao maalum zilizowaleta katika nchi zetu na hakuna jengine ispokuwa ni kazi za uhalifu. Ni watu wa kuchungwa sana kwani usije ukadanganyika kumuona mchina anachoma mahindi ukapumbazika kuwa hiyo ni kazi iliyomleta kutoka China ajekufanya Tanzania la hasha kuna kazi maalum zaidi iliyomleta hapo ni watu wanaotumia udhaifu wa wenyeji na serikali yao katika kutimiza vitendo vyao vya kihalifu mara nyingi kwa kushirikiana na wenyeji wasio waaminifu. Ni watu hatari sana katika kutorosha rasilimali za nchi husika kinyume cha sheria wakati mwengine ni vigumu kuwabaini kwa hivyo tunaomba watanzania na maamlaka husika za serikali kuwa waangalifu sana na nyenendo za wachina la sivyo watanzania watalizwa sana. Hivi karibuni tu wa Australia wameukamata mzigo wa kihistoria wa madawa ya kulevya kutoka Hong Kong China sasa kama wanathubutu kujihusisha na vitendo vya kihalifu ndani ya Australia nchi ambayo hata nzi akiruka tayari wanamuona kwenye mitambo yao ya uchunguzi sasa vipi Tanzania? Tunaomba serikali kuwa makini na hao watu, kweli tunaziki ya wawekezaji lakini sio kweli kila muekezaji anakuja na nia njema lazima umakini uzangatiwe katika kuwabaini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...