Mabondia, Mada Maugo na Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' watapanda ulingoni kusindikiza pambano la Francis Cheka na Geard Ajetovic la ubingwa wa mabara wa chama cha WBF Februari 27.

Cheka na Ajetovic watawaniaubingwa wa super middle katika pambano la raundi 12 lililopangwa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.

Kwa mujibu wa Meneja wa Cheka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Advance Security, Juma Ndambile, Pazi na Maugo watawania ubingwa wa Afrika wa uzito wa super-middle na tayari WBF wamekwisha toa Baraka kufanyika kwa pambano hilo na watalisimamia.

Alisema kuwa siku hiyo pia, Mohamed Matumla atazipiga na Ibrahim Class katika pambano la raundi nane la uzito wa light-weight.

Ndambile alisema kuwa mapambano hayo yatasimamiwa na waamuzi kutoka Ujerumani na Afrika kusini ambao watawasili nchini Februari 23 pamoja na rais wa WBF, Howard Goldberg.

"Waamuzi  watawasili na ndege ya Afrika Kusini, Februari 23 Ajetovic atawasili pia tayari kwa pambano hilo la kimataifa," alisema Ndambile.

Cheka tayari yuko Dar es Salaam ambako amepiga kambi chini ya kocha wake, Abdallah Salehe 'Comando' kujiweka fiti na pambano hilo.

 Awali mabondia hao walizichapa 2008 nchini England na Cheka kupigwa kwa pointi mjini Manchester.
 Mapema Jana, wakati wakitambulisha pambano lao, Maugo na Dullah Mbabe walitaka kuzichapa kavu kavu kabla ya kuamliwa na Mlinzi aliyeambatana nao, Chrispin stephano.

Wakizungumzia pambano hilo, Maugo na Dullah Mbabe kila mmoja alitamba kumsambaratisha mpinzani wake watakapozichapa siku hiyo.

 "Namheshimu Dullah, ni Bondia mzuri lakini ajipange siku hiyo, hasira zangu za kukosa ubunge nitazimalizia kwake," alitamba Maugo.

Wakati Dullah Mbabe akimtahadharisha Maugo na kubainisha kwamba atamuonyesha kwa vitendo ulingoni siku hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Advanced Security Company Limited, Juma Ndambile (watatu kutoka kulia) na mratibu wa pambano la ubingwa wa mabara kati ya Francis Cheka na Msebia Geard Ajetovic Jay Msangi wa tatu kutoka kushoto, wakiwatambulisha mabondia watakaozichapa kwenye masumbwi ya utangulizi, wakati wa pambano la ubingwa wa mabara kati ya Francis Cheka na Msebia Geard Ajetovic, litakalofanyika Februari 27 kwenye viwanja vya leaders club, jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...