Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick  kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Hemed Mkali wara baada ya  kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali waliofika wakati wa mkutano wake na Wazee wa jiji la Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam  kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa


  1. Ndugu Raisi Magufuli, niwie radhi kwa kutokuita Mh......a, kwani mimi bado naona Ndugu ni bora zaidi kuliko hiyo inayotumika sasa.

    Ndugu Raisi, hotuba yako kwa wazee wa Dar na wa Tanzania kwa ujumla, ni dhihirisho murua kabisa kwamba, serikali yako ya awamu ya tano, pamoja na ndugu zetu wote katika serikali hii yako tawala, mmejipanga kutumbua majipu sugu na na mengine yana kina kirefu.

    Maulana awaongoze na awalinde katika tumbua tumbua hii, hata kama mkitumbua jipu lakini mkakuta saratani iliyovamia mifumo mingine ( metastatic carcinomas), msiishiwe nguvu, bali mtumie "mionzi", "kemikali" na "upasuaji" ili saratani hiyo ya ufisadi ilegee kama mlenda, na kutokomea kama "mkoloni" aliyepigwa na kibanga.

    Naomba ukisha anzisha mahakama maalum ya kusikiliza kesi za mafisadi, basi uanzishe kitengo kidogo sana, ambacho wananchi wanaweza kubiga simu bure (Freephone), ili kutoa taarifa za UFISADI na za MAFISADI, hii itakuwa tofauti na "Takukuru", kwani itajengwa na damu mpya, jobless lawyers, teachers, wauza vitumbua, bodaboda guys etc.

    Haya ni mawazo yangu tu, hivyo mtakao hukumu, mtoe kwanza "boriti".......

    I have fallen in Love AGAIN, with my beautiful country of Tanzania, and trust me, it feels awesome.

    Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.



    ReplyDelete
  2. MTOA MADA WA KWANZA UMENIFURAHISHA SANA,UBARIKIWE.TANZANIA ILIFIKIA HATUA YA MTU MWIZI WA MALI ZA UMMA NDIYE ANAONEKANA MTU ALIYEENDELEA ASIYEIBA ATAITWA HAFANYI KITU ,MJINGA MBUMBUMBU NK.KWA MFANO JAMAA MMOJA ALIKUWA MHASIBU WA CHUO CHETU KIMOJA CHA MAMBO YA DIPLOMASIA NA KWA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI FULANI WA WIZARANI MAMBO YA NJE.WALIFANYA EPA ZAIDI ZA FEDHA MABILIONI JAMAA AKAJENGA HOTEL MOJA YA NYOTA TATU MAENEO YA UFUKWENI KUNDUCHI. NA MAJUMBA KAMA SITA SABA HIVI MAENEO YA MASAKI NA MWENGE,SASA WATU KAMA HAWA NDIYO MAPEDESHEE HATA UKIULIZA AU UKIFUATILIA JINSI ALIVYOUPATA UMILIONIA HUU HUWEZI KUPATA JIBU SAHIHI.INAFURAHISHA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUANZA KUCHUKUA HATUA ZA KUTIA MOYO,NCHI HII NI TAJIRI SANA.KWELI TANZANIA IMEFIKIA KUWA NA NDEGE MOJA??? AIR TANZANIA MIAKA YA THEMANINI NA TISINI ILIKUWA SAFI SASA IPO TAABANI.WAKATI WATU WANAFILISI NCHI HIVI HIVI BILA HAYA.INAUMA SANA UKWELI UNABAKIA SANA KUWA TANZANIA HATUNA UTAIFA.NINAMWOMBA RAIS MAGUFULI AANGALIE SUALA LA FOLENI ZA DAR ES SALAAM SI FLYOVER NDIYO MUHIMU. MUHIMU NI BY PASS AU RING ROAD ZENYE NJIA SITA HAKUTAKUWA NA FOLENI.KENYA WAMESHAJENGA NA WANAENDELEA NA UGANDA WANAJENGA SASA SISI TUPO WAPI?????????? BARABARA YA MWENDO KASI MOROGORO ROAD IPO CHINI YA KIWANGO KABISA KABISA NA HAITATATUA CHOCHOTE,TUNAHITAJI KUBADILIKA ,MUNGU IBARIKI TANZANIA TUNAHITAJI KWENDA MBELE

    ReplyDelete
  3. Me Rais, mimi naomba nikupatie ushauri wa dhati kutoka moyoni mwangu. Kwanza mimi ni mktisto na nimesoma hitoria ikiwepo ya dini kadhaa. Hizi salamu kwamba Tumsifu Yesu Kristo hazina equivalence yake kwenye salaam ya Kiislaam AlsaamAlyekum.

    Maana ya Asalam Aleykum inayolingana kwenye Ukristo ni Amani na Iwe Kwenu or Peace be Unto You. As a Christian nashindwa kuelewa kwanini hatuitumii hiyo ambayo inalingana zaidi na Aslaaam Aleykum!

    Aidha na shangaa viongozi wa dini na wanasiasa sasa wote wameingia kwenye mkumbo ambao hauna msingi kwenye siasa zetu. Hata Mwalimu Nyerere hakuingiza mambo ya Yesu Kristo kwenye shughuli za kisiasa. Kwa ushauri wangu naomba tubadildilishe na kutumia salaam zinazolingana: Asalaam Aleykum ama Amani na Iwe Kwenu.

    Kwa unyenyekevu wa Yesu Kristo naomba kuwakilisha. Nchi yetu haina dini. Watanzania wana dini. Kila mtu ana yake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...