Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akimkabidhi  vifaa vya michezo Katibu Kata ya Mtoni kwa Azizi Ally vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke katika Hafla fupi ya kusheherekea miaka 39 ya  kuzaliwa kwa chama hicho ambapo kilele cha maadhimisho hayo yatafanyika kesho Mkoani Singida  ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Rais Mstaafu Dtk  Jakaya Kikwete
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za (CCM) Mtoni

Na Khamisi Mussa

Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ametoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke.

 Mtemvu alitoa vifaa hivyo ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kilele chake kitaifa kinafanyika leo mkoani Singida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mtemvu alisema lengo lake ni kuimarisha michezo kwenye kata hizo na kuwaepusha vijana kujiingiza katika vitendo vya kiovu na kujenga afya zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...