Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016 Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo, Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akisoma hotuba yake ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Amana lililofunguliwa Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Kijaji alimwakilisha Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Benki Amana, Dkt. Muhsin Salim Masoud, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, kuzindua Tawi hilo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...