NANI:              Amadou Gallo Fall –Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu – Africa

Allison Feaster - Mchezaji nyota na Mwandamizi wa WNBA
Paul Hinks –Mtendaji Mkuu wa Symbion Power                

NINI:               Kuanza rasmi kwa Ligi ya Mpira wa kikapu kwa vijana (Jr.NBA Basketball League) nchini Tanzani

LINI:                Saa saba Mchana, Siku ya Jumamosi; Tarehe 27,2016

WAPI:            Kituo cha Vijana cha Michezo Jakaya M. Kikwete jijini Dar es Salaam  

Shirikisho la Mpira wa Kikapu litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha JMK jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.

Sherehe hii ya ufunguzi ambayo itahudhuriwa na Mchezaji Nyota na Mwandamizi wa WNBA aitwaye Allison Feaster itakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu ya Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14. Ligi hii itajumuisha shule kutoka maeneo ya karibu zipatazo thelathini (30) kila shule ikiwakilisha moja wapo wa timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.

Wanahabari ambao watapenda kushiriki kwenye uzinduzi huu wanapaswa kutoa taarifa ( RSVP) kwa adi.raval@jmkpark.org kabla ya tarehe 25 Februari saa kumi na moja jioni. Kituo kinachoruhusiwa kushiriki kinapaswa kuwa na hadhi stahiki.

Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) Ni ligi ya NBA ya kidunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana ; wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza. Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makosha na Wazazi

Kwa maelezo zaidi kuhusu kituo cha Michezo 
cha Vijana tafadhali tembelea www.jmkpark.org.

*** FURSA ZA MAHOJIANO NA UCHUKUAJI PIA ZINAPATIKANA***
   
* * *Hii ni sherehe ya watu maalum – kama ilivyoainishwa hapo juu, Waandishi wahabari wanaohitaji kuudhuria WANAPASWA kutoa taarifa mapema (RSVP) kwa  adi.raval@jmkpark.org kabla ya kumi na moja ya siku Alhamisi ya Tarehe 25 Februari 2016 ili waweze kupewa ruhusa kabla ya sherehe. Tafadhali mtumie Adi barua pepe kama una swali lolote. 
Kwa Mawasiliano zaidi:
Pawel Weszka, NBA, pweszka@nba.com

Adi Raval, Symbion Power, adi.raval@jmkpark.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...