Wizara imepata
taarifa zisizo na ukweli zinazoenezwa na kusambazwa na watu wasiokuwa na nia
njema kwa Wizara na Serikali kwa ujumla, kuwa Wizara iliyokuwa ya Ushirikiano
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliendesha zoezi la kukusanya wasifu(CV) za
Wafanyakazi wake kwa lengo la kuwafukuza kazi.
Wizara imesikitishwa na inalaani vikali uvumi
wa taarifa hizi na inakanusha kuwa
taarifa hizi hazina ukweli wowote.
Zoezi la kukusanya
CV za watumishi ni zoezi la kawaida kwa waajiri na hufanyika Mara kwa mara kwa
lengo la kuhuisha sifa na uzoefu wa watumishi wanazopata wakiwa kazini ambapo
hatimaye huwekwa kwenye majalada yao binafsi, mwajiri anapaswa kuhakikisha
jalada la kila mtumishi lina taarifa zinazoeenda na wakati, hivyo zoezi hili
lilifanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa za watumishi wa Wizara kama
ilivyoelekezwa na mwajiri na si vinginevyo.
Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuwa CV si
miongoni mwa nyaraka zinazohitajika katika kumfukuza kazi mtumishi bali mtumishi
anafukuzwa kazi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi ambapo
taratibu maalumu za kinidhamu hufuatwa. Katika kipindi husika Wizara haina
mtumishi anayetuhumiwa kwa kosa la kinidhamu linaloweza kupelekea kufukuzwa
kazi, hivyo taarifa hizi hazina ukweli wowote.
Aidha, Wizara
inakemea vikali watu wenye tabia ya kutoa taarifa zisizo na ukweli na zenye
kupotosha umma. Vilevile Wizara inapenda kuwaasa wananchi kuheshimu sheria na
taratibu za Nchi sambamba na kutoeneza taarifa zinazotokana na vyanzo
visivyokuwa rasmi au zisizothibishwa na mamlaka husika, kwa kuwa kufanya hivyo
ni kukiuka sheria na taratibu za Nchi.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
19
Februari, 2016



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...