Bw. Prosper Manase Mwakale anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi, Willelmina Kasimbala (pichani, kilichotokea Leo ghafla jijini Dar es Salaam.
Msiba upo nyumbani Kwa marehemu kimara stop Over jijini Dar es salam. Habari ziwafikie ukoo wa Kasimbala , Rutataza, Na waliokuwa wafanyakazi wenzake Air Tanzania.
RATIBA YA KUMUAGA MAREHEMU WILLELMINA KASIMBALA.
Mwili utawasili nyumbani Kwa marehemu Kimara Stop Over leo saa Nne Asubuhi. Tutakula Chakula saa Tano. Saa sita tutakuwa
Katika Kanisa la Kilutheri Kimara.
Safari ya kwenda Kisiwani, Same itaanza saa Saba Mchana Kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika siku ya Alhamis.
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA WILLELMINA MAHALI PEMA PEPONI
- AMEN



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...