MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ameupongeza uongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA)kumpatia uanachama wa heshima na kumzawadia ekari tano za eneo la ardhi mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta ili ajenge kituo cha kuendeleza michezo nchini.
Akizungumza na Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael Kagondela katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga juzi, Madadi ambaye pia ni mwanachama wa SHIWATA alisema huo ni motisha mzuri utakaowavutia wachezaji wengine kujibidiisha kuiga nyayo za Samatta.
Alisema Samatta amefungua njia kwa wachezaji wengine ambao kuanzia sasa watajitahidi kuonesha vipaji vyao binafsi ambavyo matokeo yake vinageuka kuwa lulu katika sura ya Afrika na dunia.
Naye Katibu Mkuu wa SHIWATA, Kagondela alisema mtandao huo unaomiliki ekari 300 kwa ajili ya kujenga makazi na viwanja vya burudani na kumbi za starehe inatarajia kupata wawekezaji kuwekeza katika fani mbalimbali za michezo.
Alisema kutoka Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anna Wambura alipotembelea kijiji cha wasanii Mkuranga hivi karibuni ahadi zake za kuwapatia huduma za jamii za umeme, barabara na maji zimekuw2a kichocheo kwa wasanii kujenga nyumba zao kwa kasi.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema wameanza kutekeleza rai ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga aliyoitoa hivi karibuni akiwataka SHIWATA kuandaa tamasha kubwa mwaka huu litakalowakutanisha wasanii wa fani zote nchini.



Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Michael Kagondela (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi eneo ambalo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta atapimiwa ekari tano na kukabidhiwa na mtandao huo kwa ajili ya kujenga chuo cha wanamichezo, Mkuranga mkoani Pwani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...