TPDC imefanya kikao kazi na Madiwani na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa lengo la kutoa elimu juu ya sekta ndogo ya gesi. Kikao hicho kimefanyika katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba, Mkoani Mtwara. Aidha katika kikao hicho TPDC imewataka Madiwani kusimamia zoezi la ulinzi shirikishi katika mitambo ya Madimba na katika maeneo linapopita bomba la gesi asilia. 
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Fatma Ally (mwenye mtandio mwekundu) akipata maelezo kuhusu kiwanda cha kuchakata gesi asili wakati wa ziara ya mafunzo kwa madiwani iliyofanyika katika kiwanda cha Madimba, Mtwara

Diwani wa kata ya Madimba, Ndugu Ally Musa Sikawene akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya madiwani wa Halmashauri ya Mtwara na TPDC 
Mkurugenzi wa utafiti na uendelezaji wa mafuta na gesi kutoka TPDC, Mr. Kelvin Komba akitoa mada kwa waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Mtwara huko Madimba, Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...