VIDEO ya Lupeza ya msanii wa kizazi kipya, Ali kiba ambaye pia ni
balozi wa WILD AID Afrika yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo ikiwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchi walijitokeza kwa
wingi
katika kumuunga mkono msanii na balozi wa WILD AID Afrika,
katika uzinduzi wa video yake hiyo.
Video
hiyo iliyofanyiwa nchini marekani imezinduliwa katika Hoteli ya
Slipway
jiji Dar es Salaam huku kiba akiwataka watanzania na walimwengu
kuachana
na kujihusisha na ujangili wa kuuwa wanyama pori.
Baadhi ya wasanii waliojitokeza ni AT,
MwanaFA, Aika, Nahreel,
Vanessa,
Jux, Joh Makini, Wema Sepetu, Baraka Da Prince na wengine
wengi.
Msanii na balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’ akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) juu ya uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza jijini Dar es Salaam.
Wadu mbalimbali wakimsikiliza Msanii na Balozi wa WILD AID Afrika,Ali Saleh ‘Ali Kiba’katika uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza.jana jijini Dar es Salaam.
Msanii na Balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’akiwakabidhi CD wasanii mbalimbali na wanau wa muziki mara baada ya uzinduzi huo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...