Sasa ni wakati wa watanzania kuongea,
ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,
mtandao unaongoza nchini wataweza kuongea bure kwa saa nzima kila siku!
Kupitia ofa yake maalum kwa wateja ya Ongea Bure Deilee, wateja wa Vodacom wataweza
kuongea kwa muda wa saa moja bure kila siku.
Ili kujiunga na ofa hii ambayo haijawahi
kutokea nchini, mteja anachotakiwa kufanya ni kuongea kwa dakika 10 kila siku
kwa viwango ya malipo vya kawaida na hapo hapo atapata ofa ya kuongea kwa muda
wa saa moja bure ndani ya kipindi chote
cha ofa hii kabambe.
Ofa hii ya Ongea Bure Deilee pia imemuhusisha mwanamuziki nguli wa muziki wa
Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz, ambaye moja ya kibao chake kinachotamba
ni ‘Number One’, ambao pia ni mwito wa
simu maarufu kwa watumiaji wa mtandao wa Vodacom.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa hii,
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Ian Ferrao amesema “Ongea Bure Deilee ni ofa ya aina yake
kutolewa kwa wateja wa Vodacom popote walipo nchini. Ofa hii imebuniwa
kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa
murua!”
Aliendelea kusema kuwa Vodacom Tanzania
imedhamiria kuendelea kuvuka kile ambacho wateja wake wanakitarajia, kwa kuwaunganisha kwa viwango nafuu ambavyo
wanazoweza kuvimudu, lengo kubwa likiwa ni kuweza kuwainua
Ofa hii itatolewa kwa wateja milioni
moja wa kwanza watakaojiunga kila siku kwa kupiga *149*01# ambapo watakuwa huru
kuongea wakati wowote watakao, iwe usiku au mchana, ili mradi watakaowasiliana
nao ni watumiaji wa mtandao wa Vodacom.
“Huu ni mwendelezo wa kampeni yetu ya
Maisha ni Murua ambayo jitihada zetu
katika kuwaletea wateja ofa za kipekee na ambapo kupitia ubunifu wa kutumia
mtandao, tunawezesha maisha ya wateja wetu wote nchini kuwa murua. Kama ambavyo
tunasema siku zote, tutaendelea toa huduma zinazowawezesha wateja wetu
kuwasiliana kwa urahisi na wapendwa wao na hata katika shughuli zao za
uzalishaji mfululizo,” aliongeza Ferrao.
Kwa upande wake, Diamond Platinumz,
ambaye sasa ni balozi wa Vodacom alisema “Ninayo furaha kuwa sehemu ya kampeni
hii kabambe kutoka Vodacom. Nilipopata taarifa kwa mara ya kwanza kuhusu ofa
hii nilipata mshtuko na kusema dah, Vodacom imeleta tena bonge la ofa, kwa
hakika ofa hii itaniunganisha na
washabiki wangu, marafiki, familia na wafanyabiashara wengine”.
Aliongeza “Nitawaelezea washabiki
wangu, familia na marafiki jinsi wanavyoweza kufanya maisha yao kuwa murua
kupitia kampeni hii mpya kutoka Vodacom. Wanachotakiwa kufanya ili kujiunga na
kufurahia ofa ya Ongea Bure Deilee ni
rahisi tu, yaani ni kupiga simu *149*01#.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto) akiongea na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa promosheni ya”Ongea Deilee” Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa
muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea
jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom leo jijini Dar es
Salaam,anayeshuhudia kulia ni Balozi wa Vodacom
Tanzania,Nasibu Abdul (Diamond
Platinum)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom Tanzania,Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina
Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye
ujumbe wa jinsi ya kujiunga na Promosheni
ya “Ongea Deilee”,wakati wa uzinduzi
wa promosheni hiyo leo jijini Dar es
Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure
kila siku pindi wakiongea jumla ya
dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto)
akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
promosheni ya”Ongea Deilee”
Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku
pindi waongeapo jumla ya dakika 10 Vodaocom kwenda Vodacom, leo jijini Dar es
Salaam,wengine katika picha kutoka kushoto,Zarina Hassan, Balozi wa
Vodacom,Nasibu Abdul (Diamond Platinum)
Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...