Na Mugishagwe Zablon
Walimu wa shule za msingi binafsi za jijini Dar es Salaam jana wameanza mafunzo kuhusiana na mitaala mipya ya masomo kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na serikali hivi karibuni ambayo sasa yanafanya elimu hiyo iwe hadi darasa la 10 badala ya la saba la awali.
Akizungumza  wakati wa kufungua mafunzo ya ufundishaji kwa walimu kwa kutumia mtaala ulioboreshwa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na pili kwa shule binafsi, Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balalusesa alisema lengo ni kuboresha kiwango cha elimu nchini.
Kamishna huyo alisema mtaala huo uliofanyhiwa maboresho umeanza kutumika katika shule za msingi nchini na kinachofanyika hivi sasa ni mafunzo kwa walimu hao ambayo alisema kuwa ingawa yamechelewa lakini bado yanahitajika.
Alisema ingawa walimu wa shule za msingi za serikali wamepata mafunzo hayo lakini wale wa binafsi walikuwa bado na sasa ndio wakati wao lengo kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa viwango vya elimu baina ya shule na pia kuwa na mtaala mmoja.
Kamishna huyo alibainisha kuwa licha ya mitaala hiyo ya la kwanza na la pili kukamilika pia imeandaliwa ambayo imetayarishwa kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili ili kukidhi mahitaji ya shule zote iwe za serikali au za binafsi.
Alisema pia kulingana na mabadiliko hayo, pia kutakuwa na mitihani ya kuwapima wanafunzi wa darasa la pili ili kuzuia uwezekano wa kuwa na darasa la tatu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili kujua uwezo wa watoto kitaaluma na kuwasaidia wale ambao uwezo wao mdogo katika eneo hilo.
Pia vitabu vyote vya kiada kwa shule za msingi vitachapisha na kusambazwa na TIE “Msingi wa utungaji, uchapaji na usambazaji wa vitabu vya kiada kwa shule za msingi nchini unatokana na kauli ya Rais John Magufuli ya kutaka vitabu vya masomo msingi nchini kuchapwa na taasisi hiyo  ili kudhibiti upotoshaji na kuhuisha elimu nchini” alisema.
Profesa Balalusesa alisema kinachofanyika sasa sio kuandika mtaala mpya isipokuwa kuufanyia maboresho ule wa mwaka 2005 ili uendane na mabadiliko ya sasa ambayo yanataka elimu msingi iwe hadi darasa la 10 badala ya la saba
Alibainisha kuwa awali ulikamilika mtaala wa darasa la kwanza na pili na hivi karibuni wa la tatu na nne na itaendelea hivyo hadi kufikia kulikokusudiwa ambako ni kuwa na mtaala ambao utaunganisha elimu ya msingi na sekondari kabla ya kuelekea hatua zaidi.
Awali akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Ofisa Eimu Wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas alisema wilaya ya Ilala imeamua kuwashirikisha waimu wa sule binafsi pia kutokana na ukweli kuwa ni wadau wakubwa wa elimu hususan jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Eimu Wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kwa walimu ya jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  kwa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba kama ilivyokuwa awali ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIA), Albert Katagira akizungumza akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa walimu wa shule binafsi,  jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 
 Walimu wa shule za sekondari za binafsi, wakifuatilia semina ya mafunzo kwa walimu jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balalusesa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa walimu wa shule binafsi, jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Picha zote na Mugishagwe Zablon

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...