Hospital Mpya iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka vyuo vya UTAH (Moran aye Centre) na Chuo cha Weil Cornell Medicine vyote vya nchini Marekani wanatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya macho. 
Vifaa vya Kisasa kabisa na madaktari bingwa hawa watakuwepo kuanzia tarehe 22 hadi 25 mwezi huu wa pili 2016.Huduma hizi zinatolewa bure kabisa. Hii ni kutoka na Mahusiano yaliyopo kati ya Chuo Kikuu cha Dodoma na vyuo hivi. 
Watu 300 wanatarajiwa kupata  huduma ya upasuaji kwa kipindi hiki. Katika Mahojiano na Dr. Jeff kutoka Chuo Kikuu cha UTAH (Moran aye Care alisema kuwa wanafanya huduma hizi pia nchi nyingi lakini kwa Dodoma tatizo ni kubwa zaidi. Alieleza kuwa mpango wao kwa sasa ni kuja Dodoma mara mbili kwa mwaka. 
Pia wanasaidia sana katika kuwafundisha madaktari wetu wa kitanzania na hadi sasa Dr. Frank ambaye ni mwalimu katika Chuo cha afya cha Chuo Kikuu cha Dodoma amefaidika na mafunzo hayo na tayari anafundisha madaktari wengine. 
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
 Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa
Madaktari bingwa kutoka Marekani wakishirikiana na madaktari wa hapa nchini wakitoa huduma za upasuaji katika Hospital Mpya ya Benjamin Mkapa iliyopo  Chuo Kikuu cha Dodoma ya Benjamin Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Inafurahisha sana kuona misaada kama hii
    Lakini inafurahisha zaidi kuona anayekusaidia akufundisha ujisaidie mwenyewe baadaye. I am talking of their teaching of our own professionals. Wahenga wasema:Give a man a fish and you feed him for a day, teach him to fish and you feed him for a lifetime (maimonides)

    ReplyDelete
  2. This is a good thing.
    Hope we will have our own doctors performing more.
    Uhusiano huu uendelee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...