WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angela Kairuki amemsimamisha  kazi aliyekuwa mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Said Nassoro kutokana na kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake.
Kairuki ametoa maamuzi hayo leo jijini Dar es Salaam  katika mkutano na waandishi  wa  habari katika moja ya kumbi zilizopo katika ofisi za Utumishi wa Umma.

“Namsimamisha Bwana Said Nassoro aliyekuwa mkuu wa chuo hiki kwa kushindwa kusimamia watumishi walioko chini yake  na kupelekea suala zima la usimamizi wa shughuli za chuo hususani katika matawi yake mbalimbali yaliyoko mikoani kuathirika,” alisema Mhe. Kairuku.

 Kairuki aliongeza kwa kusema kuwa usimamizi  wa Bw. Nassoro  ambao haukuwa wa ufanisi umetoa mwanya kwa viongozi mbalimbali wa matawi kufanya ubadhilifu wa mali za Umma ambapo mwaka  2011 na 2013 aliyekuwa mkurugenzi wa chuo upande wa tawi la Mtwara Silvanus Ngata aliongeza gharama za ujenzi.

Aidha taarifa kutoka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU zilithibitisha ubadhilifu huo lakini mkuu huyo wa chuo hakuweza kuchukua hatua yoyote badala yake alimuhamisha Bw. Ngata kwenda kwenye tawi la Tabora na kuendelea na wadhifa wake.

Kutokana na ubadhilifu huo imempelekea  Kairuki  kumsimamisha kazi Bw. Ngata ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora na Bw. Joseph Mbwiro kutokana na matumizi mabaya ya fedha za malipo ya ada kiasi cha shilingi bilioni moja ambazo zilikuwa zikilipwa na wanafunzi kwa mwaka wa fedha 2014/15.

Kairuki ameendelea kueleza kuwa  bado wanaendelea kuondoa watumishi wa Umma ambao hawafuati   mifumo na miongozo ya Utumishi wa Umma ili kuwabakiza  watumishi ambao wanaonyeshe taswira nzuri na kufuata mifumo na  miongozo  ya Utumishi wa Umma kwa ukamilifu wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Fashion kufukuzishwa kazi haya

    ReplyDelete
  2. Vizuri kuwajibika. Bibi Angela Kairuki ni mwenye hekima na mchapa kazi ndiyo manake Rais wetu alimteua kuwa waziri kamili. Mungu azidi kukubariki

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...