Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna ( wa pili kutoka kulia) akielezea majukumu ya kampuni hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zilizopo chini yake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akielezea fursa za uwekezaji katika sekta ya gesi nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Pan African Energy Andy Hanna (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Pan African Energy Nchini Patrick Rutabanzibwa (kulia) wakinukuu maelekezo kutoka kwa Wiziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kufanya kazi katika mtindo wa kisasa ili nishati ya umeme iweze kuwa ya uhakika kwa maendeleo ya uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo aliyasema hayo katika kikao chake na Kampuni ya Pan African Energy kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilichoshirikisha pia watendaji kutoka wizara ya nishati na madini, TANESCO, TPDC na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Ni aibu kuona Kenya inazalisha umeme mwingi kuliko Tanzania. Kenya inazalisha umeme wa geothermal energy. Lakini Tanzania tumelala.
ReplyDeleteSisi tuna kila kitu.Bonde la ufa lipo. Makaa ya mawe yapo. Maji yapo. Gas ipo. Jua lipo. Upepo upo. Uranium ipo. Lakini bado hatuna umeme wa kutosha na wa ziada. Wataalamu wa mipango na uchumi wa mashirika kazi yenu ni nini? Mbona tunapata aibu ya bure?