Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo ametaka kasi iongezwe katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha uchakataji na usindikaji wa gesi kimiminika unaotarajiwa kuanza mkoani Lindi mara baada ya taratibu za maandalizi kukamilika.
Profesa Muhongo alisema hayo katika kikao kwa ajili ya kujadili hatua iliyofikiwa ya maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho kilichoshirikisha watekelezaji wa mradi huo ambao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) na makampuni yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini.
Makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo ni pamoja na Shell, Statoil, Ophir Energy, Pavilion na Exxon Mobil. Pia kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
Mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata na kusindika gesi kimiminika Profesa Muhongo alilitaka shirika la TPDC kushirikiana kwa karibu na makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi yanayotekeleza mradi huo na kwa kasi ya haraka ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...