Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kati yake na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger. Pia kikao hicho kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na taasisi zake likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa na teknolojia kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Na
Greyson Mwase, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametaka makampuni
yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kuongeza kasi ya
utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili sekta ya gesi na mafuta iweze kukua na kuchangia
ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa
Muhongo alitoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na
usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger yenye makazi yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Kikao
hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka Wizara
hiyo pamoja na taasisi zake likiwemo
Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la
Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) na Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Alisema Tanzania kwa sasa ina utajiri mkubwa wa rasilimali ya
gesi ambayo itachochea
katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia umeme wa uhakika utakaotumika katika
viwanda na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.
Aliendelea
kusema kuwa ili sekta ya gesi na mafuta
iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji
wawekezaji watakaowekeza kwa kasi kwa
kutumia teknolojia ya kisasa.
Alisisitiza
kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya
gesi na mafuta kwa kutumia teknolojia ya
kisasa.
“
Kama serikali tumedhamiria kuhakikisha
kuwa Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zenye utajiri unaotokana na rasilimali
za gesi na mafuta, hivyo tunapenda
kushirikiana na wawekezaji kutoka sehemu
mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kutumia
teknolojia ya kisasa,”
alisema Profesa Muhongo
Profesa
Muhongo aliihakikishia kampuni ya Schlumberger kuwa serikali itafanya kazi kwa karibu nayo na
kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili sekta ya gesi na mafuta iweze kukua kwa kasi na
kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Awali
akizungumza katika kikao hicho Meneja Masoko
kutoka kampuni ya Schlumberger,
Abdul Adeshina alisema kampuni yake
imekuwa imekuwa ikitoa mafunzo
kwa wafanyakazi wa kitanzania asilimia
80 wanaofanya kazi katika kampuni
hiyo.
Aliongeza
kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana
kwa karibu na Shirika la Maendeleo ya
Petroli Nchini (TPDC) katika shughuli za utafiti wa mafuta na gesi nchini na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ipo tayari kutumia teknolojia na vifaa vyake katika kuboresha shughuli za
utafutaji wa mafuta na gesi nchini.


Tunafurahishwa mikutano kama hii kujumuisha vitengo vyote ambavyo ni wadau wa sekta husika. Ufahamu wa pamoja utarahisha kufanya maamuzi kwa haraka na kushauriana miradi ya kutekeleza kwa pamoja. Hii ndio safi. Tanzania mpya ileee. Tuwashauri Tanesco na TTCL na DAWASCO na Tanroad wakae chini wakubaliane sehemu za kupitisha mabomba yao. Maana kuna mchezo wa ajabu. Utakuta barabara inajengwa DAWASCO wapo wanatazama. Lakini ikiisha tu. Utaona wanachimbua higo barabara eti kupitisha mabomba ya maji. Hivi wakati barabara zinajengwa wanakuwa wapi! Kama kunahitaji basi itengenezwe mifumo maalum ya kupitisha mabomba kukatisha barabara bila kulazimika kuchimbua na kubomoa sehemu ya barabara. Hivyo hongera Sospeter kwa kuwakutanisha hawa wadau.
ReplyDelete