Ni baada ya kumalizika dakika 90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga, uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam na  timu ya Yanga kuibuka kidedea baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34 kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.
PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban akiwa amejiweka tayari kuokoa mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba, Kessy Ramadhan, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...