Makamu Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
NA VICTOR MASANGU, PWANI
IMEELEWA kwamba kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimeweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara na madaraja katika baadhi ya maeneo ya mkoani Pwani hali ambayo imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi kutokana na magari kukwama hivyo kutokupitika kwa urahisi.
Hayo yamesemwa na Mhandisi mkuu wa kitengo cha mipango kutoka Wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Zuhura Amani wakati akiwakilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za matengenezo na miradi ya maendeleo kwa wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa, ambapo amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu hiyo kunarudisha nyuma jitihada za serikai katika kuleta huduma kwa jamii.
Zuhura alisema kuwa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 20.9 zilipangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014 hadi 2015 lakini kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti zoezi hilo halikuweza kufanikiwa kwa wakati uliopangwa.
Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya miundombinu ya barabara.
Kwa upande wao wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho akiwemo Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya ya Kibaha Mji,Maulid Bundala pamoja na Katibu msaidizi wa Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala walisema hai hiyo ya ubovu wa barabara inachangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa magari hivyo kupelekea usumnufu mkubwa hasa katika kipindi cha mvua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...