Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Barcelona ya nchini Uhispania imefanikiwa kuvunja ‘record’ iliyowekwa kwa takliban miaka 27 ya Ligi Kuu Soka nchini humo,baada ya kucheza michezo 35 bila ya kufungwa.

Barca imevunja record hiyo baada ya hapo jana kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Rayo Vallecano katika mchezo wa Ligi Kuu maarufu kama La Liga.

Katika mchezo huo, Lionel Messi  alifanikiwa kufunga mabao 3 peke yake(hat-trick) ikiwa ni ya 35,na kufikisha mabao 33 katika msimu wa Ligi,huku mabao mengine ya Klabu hiyo yakifungwa na Ivan Rakitic pamoja na Arda Turan.

Washambuliaji wa Rayo,Diego Llorente and Manuel Iturra  walishindwa kutamba katika mchezo huo mbele ya Barca,wakati bao lao la pekee likifungwa na Manucho.
Kwa matokeo hayo,Barca inafikisha points 69,huku Atletico Madrid ikiwa na points 61 wakati Real Madrid ya Zinedine Zidane ina points 57.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...