Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim, Bw. Selemani Ponda (katikati) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kutangaza kuingia kwa benki hiyo nchini Uganda na kuweka rekodi ya kuwa benki ya kwanza ya Kitanzania kuingia nchini humo. Wengine ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bw. Abdulrahman Nkondo (kushoto) na Meneja Mwandamizi Huduma kwa Wateja, Bw. Frank Matoro.

BENKI ya Exim Tanzania imezidi kajitanua nje ya mipaka ya nchi baada ya kufanikiwa kuingia rasmi nchini Uganda na kuweka rekodi ya kuwa benki ya kwanza ya Kitanzania kuingia nchini humo.

Mafanikio hayo yamekuja baada ya benki hiyo kutwaa asilimia 58.60 ya hisa za iliyokuwa benki ya Imperial ya Uganda. Hatua hiyo inapelekea benki hiyo kutambulika kama ‘Exim Bank Uganda Ltd’ nchini humo huku ikihusisha wamiliki wenza wawili ambao ni kampuni ya Amazal Holdings (maarufu kama ‘Mukwano Group’) yenye hisa 36.7%  pamoja na kampuni ya Export Finance Ltd yenye hisa 4.9%.

“Tunayo furaha kuwatangazia wana Afrika Mashariki kwamba Benki ya Exim imefanikiwa kuingia nchini Uganda ikiwa katika ushirikiano na makampuni makubwa na yanayoheshimika nchini Uganda,’’ alisema Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Bw Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Aliongeza kuwa ushirikiano huo umekuja wakati muafaka ikiwa ni kipindi ambacho nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pia zimeongeza ushirikiano ili kuwa na nguvu ya pamoja.

Akizungumzia uendeshwaji wa benki ya Exim Uganda Bw Ponda alisema kwa kuanzia benki hiyo itaanza na matawi matano jijini Kampala ikiwa na rasilimali (asset) yenye thamani ya takribani dola za kimarekani milioni 100.

“Makao makuu ya benki yatakuwa barabara ya Hannington na kwa kuanzia tutakuwa na zaidi ya wafanyakazi 100 walio na ari ya kutimiza majukumu yao ambayo ni kuhudumia wateja wetu wakubwa na wadogo kwa kuwa benki hiyo itatoa huduma zote za kibenki,’’ alibainisha.

Kuingia kwa Benki ya Exim nchini Uganda kunaifanya izidi kusimika mizizi yake kwenye ukanda wa Afrika mashariki na hivyo kuzidi kutoa mwanga wa kutimiza lengo lake la kuwa muhimili imara kwenye huduma za kibenki katika ukanda huo.
Benki hiyo ambayo kwa sasa ina rasilimali ya Sh trilioni 1.259 (Dola za kimarekani milioni 580) inatarajiwa kutimiza miaka 19 ifikapo mwezi Agosti mwaka huu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini huku kwa sasa ikiwa ina jumla ya matawi 30 nchini na matawi mengine 9 nchini Comoro na Djibout. Kuingia kwake nchini Uganda kunaongeza idadi ya matawi ya benki hiyo nje ya nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...