Na Mdau Ughaibuni
Tangu JPM aingie madarakani amekuwa akifanya maamuzi ya haraka kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wanyonge wa Tanzania. Naamini amekuwa akifanya hivyo ili kuwaonyesha njia viongozi wengine wa chini yake ili nao wawe wabunifu, wenye uthubutu, na waweze kufanya maamuzi ya haraka ili kuwapunguzia shida watanzania wanyonge.
Swali ninalojiuliza, Je viongozi wa chini yake wanaliona hilo na kufuata mfano wake. Tumewaona wachache wanaojitahidi lakini wengine sina uhakika kama watafikia matakwa ya Rais wetu mpendwa. Nachelea kusema haya kwani viongozi wasio wabunifu, wanaofanya kazi kwa mazoea na wasio na uthubutu wataendelea kumchosha Rais na Waziri mkuu wetu na kuchukua muda wake mwingi kufanya maamuzi ambayo yangefanywa nao katika ngazi zao. Ni vyema Rais na Waziri mkuu waachwe wafanye mambo makubwa zaidi katika ngazi yao.
Je, Viongozi wa Wizara ya Afya walikuwa hawaoni kuwa wakina Mama wanalala chini mpaka Magufuli aje? Kama waliona walichukua hatua gani? Ni jambo la wazi Kwamba hali ilivyo kuwa Muhimbili ni hivyo ilivyo katika hospitali nyingine mikoani na wilayani na viongozi wapo. Unategemea Rais au Waziri mkuu watembelea hospitali za wilaya zote ndio mambo yabadilike. Ni vyema viongozi wa ngazi hizo waende na spidi ya JPM na kama hawawezi basi , ameshasema mwenyewe kwamba wampishe.
Muda wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha. Mfano mzuri ni kuhusu askari wa usalama barabarani, wanaona dhahiri vijana wa bodaboda wanavunja sheria kwa kuvuka taa nyekundu, hawafuati miongozo ya taa za barabarani na mara nyingi wanasababisha ajali. Akari polisi wanasubiri mpaka ajali itokee na sio kuzuia ajali isitokee. Kuna siku moja niliwauliza askari wa usalama barani kwa nini hawawakamati waendesha bodaboda wanaovunja sheria kwa kuvuka kwenye taa nyekundu? Kwa mshangao askari huu alinijibu hawa hatuwawezi labda tuwapige risasi. Utaona kabisa ubunifu katika utendaji kazi wake hakuna kabisa. Siku moja nilitembelea chuo kikuu kimoja jjini DSM katika idara inayoshughulikia maji na mazingira. Idara hii ndio unayofundisha wahandisi wa maji na mazingira, Lakini cha kushangaza katika ofisi yao hakuna maji ya bomba wana weka maji kwenye ndoo kwa ajili ya chai na kutumia maliwatoni. Kwa kweli kilinishangaza kidogo, hawa ndio wataalam wenyewe wanaofudisha taaluma za maji lakini wenyewe wanashindwa kujiwekea maji ya bomba yanayofanya kazi ndani za ofisi zao, sasa wanafundisha nini? Utaona hapa ni kufanya kazi kwa mazoea na kukosa ubunifu. Mifano ni mingi. Mheshimiwa JPM una kazi kubwa sana ya kubadilisha mfumo. Ikiwezekana baadhi ya wafanyakazi wa serikali wastaafishwe mapema ili uweke damu mpya yenye ubunifu na uthubutu. Kuna watanzania wengi wako nje wameajiriwa na mashirika ya kimataifa wako tayari kuja kuijenga nchi chini ya uongozi wako imara. Ikiwezekana nao warudishe nyumbani waje wachangie uchumi wa taifa. Naamini ukijenga mfumo wa uwajibikaji na ukaweka damu mpya katika ngazi zote ma DC, RC, Wakurugenxzi wa wilaya na idara za serikali utaivusha Tanzania haraka kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Mungu ibariki Tanzania
Maoni matamu kabisa yamejaa uzalendo.
ReplyDeleteWahenga walisema "Mgeni njoo wenyeji wapone", hao waliozowea kufanya kazi kwa mazowea kubadilika kwa leo na kesho sidhani kama itakuwa rakhisi, maana siku zote mazowea yana tabu, mazowea hujenga tabia na tabia haina dawa. Lakini kwa juhudi, jitihada na kasi ya Mh. Rais wetu JPM aliyoanza nayo, itabidi tu wachaguwe moja, kusuka au kunyowa kwa manufaa ya watanzania na Taifa zima kwa jumla. Mungu ibariki Tanzania na watu wake, ibariki Afrika na dunia kwa jumla.
ReplyDeleteHilo la bodaboda huwa linanishangaza sana. Wako juu ya sheria, yaani hili ni jipu lingine.
ReplyDeleteSwala lingine ni uhalifu, nilishawahi kulisema huko nyuma wakati wa JK, likapita sikio moja likatokea upande wa pili. Kwa JPM naamini wataliona hili. Nilishauri hivi, mabalozi wa nyumba kumi warudishwe na wapewe posho. Wasiwe viongozi wa CCM kama zamani bali bali sehemu ya serikali ya mtaa. Kila mgeni anayekuja eneo lake kwa zaidi ya siku tatu lazima ajulishwe. Akiona watu wa ajabuajabu eneo lake atoe taarifa. Itasaidia sana kama ilivyokuwa enzi za Nyerere.