JAJI mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (wa pili kulia) akifuatana na maafisa ya jeshi la Magereza Pemba wakati alipowatembelea mahabusu na wafungwa katika Gereza na Wete Pemba kufahamu matatizo mbali mbali yanayowakabili
MMOJA ya wazee wa Mahakama ya ardhi Chake chake Pemba Khamis Mzee akielezea matatizo mbali mbali yanayoikabili mahakama hiyo katika utendaji wake wa kazi za kila siku, wakati jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu alipofanya zaira katika mahakama hiyo.
 MRAJISI wa Mahakama kuu Zanzibar Mhe. George Kazi (kulia) akichambua mambo mbali mbali yanayofanywa katika Mahakama ya mwanzo Wete
 AFISA wa kitengo cha komputa (IT) Mahakama za Pemba Mohamed Juma (kulia) akimfahamisha jambo Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, juu ya utendaji kazi wa komputa za Mahakama ya Wete  wakati wa ziara yake Mahakamani hapo
 MKURUGENZI wa baraza na mji Wete Mgeni Othman aliyesimama akielezea matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya Mwanzo Wete, wakati jaji mkuu wa Zanzibar alipofanya ziara Mahakamani hapo
AFISA Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji, Makaazi na Nishati Pemba Hemed Salum Hemed akizungumzia matatizo mbali mbali yanayoikabili Mahakama ya ardhi Wete, wakati wa ziara ya jaji mkuu katika Mahakama hiyo. Picha zote na Picha na Ameir Khalid

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...