Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhem Meru
amekutana ujumbe wa Jumuiya ya Mabohora kutoka Mumbai nchini India wenye lengo
kuwekeza katika sekta ya Viwanda nchini.
Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu Dkt. Meru aliwakaribisha na
kuwahakikishia uwepo wa mazingira bora na wezeshi kwa ajili ya uwekezaji Tanzania.
“Tanzania ina malighafi nyingi kuanzia madini, mazao ya chakula, mbao, Samaki na
kadhalika, tunawaomba mfike kwa wingi ili mje kuwekeza katika sekta ya Viwanda.”
Katibu Mkuu Dkt. Meru alisema dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
viwanda vinakuwa ni daraja la kubadilisha uchumi wa Tanzania kuwa wa kipato cha
kati.
Alisema kuwa Sekta ya Viwanda ina jukumu kubwa la kuchangia pato la Taifa kwa
asilimia 15 na vile vile kuongeza ajira kwa vijana hadi kufikia asilimia 40.
“Kuwepo kwenu leo mahali hapa kunatia moyo ya kuona dhamira ya Serikali ya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda inawezekana.”
Awali mwenyeji wa Jumuiya ya Mabohora nchini Bw. Murtaza Adamjee alimweleza
katibu Mkuu lengo lao safari yao ni kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya
viwanda hususani.
Bw Adamjee aliongeza kuwa jumuiya hiyo itawekeza katika viwanda vya kutengeneza
ngozi na viatu, nguo na mavazi, vifungashio, pamoja na viwanda vya chuma isiyoshika
kutu.
Aidha Jamii ya Mabohora walitaka kuwepo na mawasiliano, kubadilishana uzoefu na
ujuzi katika sekta ya viwanda na kuwaalika watanzania kutembelea India kuona
maendeleo ya viwanda nchini India.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Adelhem Meru wa nne (kulia), Naibu katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda, Mhandisi Joseph Malongo wa tatu (kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na ujumbe kutoka Jumuiya ya Mabohora kutoka nchini India waliotembelea wizarani mapema
leo wakiwa na dhamira ya kuwekeza katika sekta ya Viwanda. Kulia kwa Katibu Mkuu ni Bw. Murtaza
Adamjee Mkururugenzi wa kampuni ya Global Group ambaye pia ni mwenjeji wa ugeni huo.
Katibu Mkuu Dkt.Adelhem Meru akimsikiliza kwa makini Bw.Murtaza Adamjee alipokuwa akiwatambulisha wageni alioongozana nao katika ziara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara akizungumza na vijana kutoka nchini India ambao
wameonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya Viwanda.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Mhandisi Joseph Malongo, akimsikiliza
kwa makini mmoja wawekezaji kutoka jumiya ya Mabohora waliotembelea Wizarani mapema hivi leo.
Kwa wanaotaka kuwasiliana kwa biashara na wajumbe hao, tumia 0784 430 787 kwa ajili ya appointment. Wapo hadi mwishoni mwa wiki
ReplyDelete