Kampuni ya simu tanzania ttcl, imetoa msaada wa vyakula na vinywaji kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya pasaka. Msaada huo umetolewa kwa vituo vya friends of don bosco cha kimara suka ,kituo cha honoratha cha temeke na kituo cha green pastures cha bunju vyote vya jijini dar es salaam.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa ttcl dr kamugisha kazaura, meneja uhusiano wa TTCL bw nicodemus thomas mushi amesema, ttcl inawathamini watoto wanaoishi katika mazingira magumu na mara zote imekuwa ikijitahidi kuwasaidia ili kuwapunguzia magumu wanayopitia na kuwapa tumaini la maisha.

Msaada huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kusaidia jamii. Takribani watoto 300 wa vituo hivi watanufaika.. Watoto hawa ni wetu, ni sehemu muhimu ya jamii yetu, ni tegemeo la nguvu kazi ya taifa letu siku zijazo. Kwa kuwaonesha upendo, tunawatia moyo na kuamsha ari ya kujituma katika masomo ili waweze kutimiza ndoto zao na baada ya masomo waweze kujitegemea na kuwa raia wema wa nchi yetu, amesema bw mushi.

Misaada iliyotolewa ni mbuzi 3, kilo 300 za mchele, kilo 300 za unga wa sembe, kilo 150 za maharage, ndoo kubwa 6 za mafuta ya kula, katoni 60 za vinywaji( maji, juisi na soda) na viungo mbali mbali vya chakula.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya watoto na walezi wa vituo vilivyosaidiwa, mkuu wa kituo cha green pastures mchungaji douglas kiseu amesema, msaada wa ttcl ni faraja kubwa kwao kwani unawawezesha watoto kufurahia sikukuu kama wenzao walio na wazazi na walezi, na kuwapa fursa ya kutulia, kuelekeza mawazo na juhudi zao katika masomo na mafundisho ya stadi mbali mbali zinazotolewa vituoni humo.

Akishukuru kwa niaba ya wenzake, mtoto elizabeth mapunda amesema, jamii inao wajibu mkubwa wa kuwasaidia wahitaji ili kutimiza maagizo ya mwenyezi mungu yanayowataka wenye uwezo kuwa msaada kwa wanaopungukiwa. Watoto wote wenye mahitaji tunamshukuru rais john pombe magufuli na mama janeth magufuli kwa kuonesha mfano mwema wa kutujali na kuwa mstari wa mbele kutusaidia na tunaziomba taasisi za umma na binafsi kuunga mkono juhudi hizo kama ttcl inavyofanya mara kwa mara.
Mchungaji Douglas Kiseu wa Kituo cha Green Pasture akipokea msaada wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya pasaka kutoka kwa Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi.
Mwakilishi wa Kituo cha Honoratha cha Temeke akipokea msaada wa vyakula kwa ajili ya pasaka kutoka kwa Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi.
Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vitatu (3) vya jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kuwafanikisha kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...