![]() |
| Mlinda Mlango wa Mbeya City, Juma Kaseja |
Kocha mkuu wa Mbeya City Fc , Kinnah Phiri amesibitisha kuwa mlinda mlango mahiri wa kikosi chake Juma Kaseja hatakuwa sehemu ya nyota watakaoiwakililisha Mbeya City kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Simba Sports club uliopangwa kuchezwa Jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.
Muda mfupi uliopita kocha Phiri ameudokeza mtandao huu kuwa ilikuwa waungane na kipa huyo leo asubuhi kwenye kambi ya muda hapa Morogoro lakini imemlazimu kumuongezea muda zaidi wa kukaa karibu na familia yake ili kushughulikia masuala kadhaa ya kifamilia aliyonayo hivi sasa.
“Wakati anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia yale yote yaliyopo kwenye familia yake na imani yangu kuwa ataungana na kikosi mara tu tutakaporejea mbeya kujiandaa na mchezo dhidi ya Stand United March 10.
Juma Kaseja aliondoka jijini Mbeya mara baada ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prison uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine kufuatia taarifa njema ya mkewe kujifungua watoto mapacha.
Wachezaji wanzeke na uongozi wa City kwa ujumla unampongeza Juma Kaseja na kumtakia kila la kheri kwenye malezi ya watoto wake.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...