MBUNGE wa Busanda (CCM) LOLENSIA
BUKWIMBA ameeleza furaha yake kwa kamati maandalizi ya Tamasha hilo ambalo halikuwahi kufanyika
mkoani humo na imekuwa faraja kwake kama mwakilishi wa wananchi wa mkoa huo unaokabiliwa na mauaji kwa walemavu wa ngozi.
Alisema
amefurahishwa kufanyika kwa tamasha hilo mkoani Geita na mikoa mgine kwani ana imani wakazi wa mkoa huo
watahamasika kuacha mauaji ya Watanzania
wasio na hatia ambao ni walemavu wa ngozi na vikongwe ambayo yanaendelea. Mbunge
huyo anaelezea furaha yake, ana imani wananchi wa mkoa wa Geita watafurahi
kwa sababu mkoa huo umesuswa kwa kuwapelekea matamasha ya namna hiyo na kusikia
yanafanyika katika mikoa mingine kama Dar es Salaam na Mwanza.
“Nimefurahi
sana Msama kulileta Tamasha hili litakalopiga vita mauaji ya vikongwe na
walemavu wa ngozi, nina imani wananchi wataweza kuelimika kwa njia moja au
nyingine, baada ya hapo inawezekana kabisa likaweza kubadilisha fikra na
mtizamo juu ya suala hili na kupunguza kabisa mauaji haya,” anasema Lolensia.
Alieleza
kuwa limekuwa jambo la bahati kwa mkoa huo kufikiwa na tamasha hilo ambalo lina
mafanikio makubwa katika kutimiza malengo yanayokusudiwa hivyo anaamini
kilichokusudiwa kwa Geita kitafanikiwa kwa kiasi kikubwa. “Tunawakaribisha sana na nichukue nafasi ya
pekee kumpongeza Msama kwa uamuzi wake wa kutuletea tamasha hili tunatarajia
kupata mambo makubwa pia nina imani wanageita watafurahia mno kwasababu
wanapenda mambo hayo ya muziki hasa huu wa Injili,” alisema Lolensia.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...