Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155, Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.
Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.
Mhe. William Lukuvi akipokea msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao Makuu ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu TGGA.
Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe. Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni Chakula, Nguo , viatu na Madaftari.
Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa.
Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...