Naibu Balozi wa Ujerumani, John Reyels, (kulia) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Katika hoapitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Profesa Mohamed Janabi (kushoto) baada ya naibu balozi huyo kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo jana. Katikati ni Rais wa Rotary Club  Dar es Salaam, Zainul Dossa.
 Naibu Balozi wa Israel, Nadar Peldman akizungumza na madaktari, wauguzi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada ya kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Muhimbili. Jana watoto wanne walifanyiwa upasuaji na leo watoto sita wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwenye taasisi hiyo.  
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi, akishukuru mabalozi, wawakilishi wa BAPS Charities, madaktari kutoka Israel na wadau wengine kwa misaada mbalimbali ambao wamekuwa wakisadia kufanikisha shughuli za upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa  shirika lisilo la kiserikali la Save  Child’s  Heart (SACH), Simon Fisher kutoka nchini Israel akizungumza leo baada ya kufuatilia shughuli ya upasuaji wa watoto ambayo imeanza jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili. Kushoto ni Rais wa Rotary Club nchini Tanzania, Sharmila Bhatt. 

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari akiwashukuru wadau hao wakiwamo mabalozi kutoka Israel na Ujerumani na wadau wengine kwa misaada mbalimbali wanayoitoa katika taasisi hiyo. Leo Profesa Bakari amewataka madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo kutumia vizuri nafasi mbalimbali za mafunzo kutoka kwa wadau hao wa afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...