Na Bashir Yakub. 

 Makala haya yanaeleza wakati ambapo ndugu anafariki huku akiacha shauri mahakamani ambalo alikuwa akidai kitu fulani kama haki yake. Yaweza kuwa alifungua kesi kudai ardhi, nyumba, mirathi, mgogoro wa kimkataba, fidia, na madai mengine yote. 

Makala yatatizama uwezekano wa ndugu kuendeleza madai haya ili kuona namna ya kupata kile alichokuwa akidai marehemu. 

 1.ISEMAVYO SHERIA. 

Amri ya 22 kanuni ya 1 – 12 Sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai ndiyo inayozungumzia jambo hili. Katika kanuni hizo si tu imezungumzwa haki ya marehemu mlalamikaji bali pia haki ya marehemu mlalamikiwa/mdaiwa. 

 Kanuni ya 1 inasema kuwa kifo cha mlalamikaji/mdai au mlalamikiwa/mdaiwa hakiui shauri ikiwa haki ya kulalamika bado haijafa. Maana yake ni kuwa kuna wakati mdai anakufa lakini haki yake ya kuendelea kudai alichokuwa akidai inaendelea kuishi na kuna wakati akifa anakufa na haki yake ya kudai. Ni wakati gani akifa anakufa na haki yake ya kudai na ni wakati gani akifa haki yake inaendelea kuishi tutaona hapa chini. 

2. KUENDELEA KUISHI KWA HAKI YA MADAI NA KUFA KWA HAKI YA MADAI. 

Kuendelea kuishi kwa haki ya madai maana yake ni kuwa ndugu wa marehemu hasa msimamizi wa mirathi anapata haki ya kuendeleza shauri na kudai kilekile alichokuwa akidai marehemu. Na kufa kwa haki hiyo maana yake ni kuwa hakuna ndugu yoyote kutoka upande wa marehemu akiwemo msimamizi wa mirathi atayekuwa na haki ya kudai au kuendeleza shauri ili kupata kile alichokuwa akidai marehemu. 

 Hali ni hiyohiyo kwa upande wa mlalamikiwa/mdaiwa aliyefariki. Kwani kuna wakati ndugu watalazimika kurithi shauri ambalo alikuwa ameshitakiwa nalo na kuna wakati hawatalazimika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...