WAZEE na walemavu wa viungo wanaoishi katika mazingira magumu katika kambi ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi mkoani hapa, wamekumbukwa kwa kusaidiwa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 54.
Hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ilifanyika jana mbele ya mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli katika kambi hiyo yenye watu wenye mahitaji mbalimbali ya kijamii.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alivitaja vifaa vilivyotolewa kuwa ni Mchele tani 6, Unga wa mahindi 6, Maharagwe tani 3, Sukari tani 2 na nusu na mafuta ya kula lita 1000.
Dk. Kimei alitaja vifaa vingine vilivyotolewa katika kambi hiyo ya wazee kuwa ni pamoja na umeme wa jua na kudai kwamba hatawataishia hapo wataendelea kutoa misaada ikiwemo kukarabati majengo ya makazi hayo.
Kwa upande wake, Janet Magufuli, alisema kuwa katika kipindi kichache alichozunguka katika kambi 17 nchini alikuta kambi hizo zinakabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo ya maladhi.
Alisema kuwa hali hiyo ilisababisha kuanza kutafuta wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo ambayo ilichukua jukumu hilo la kuwasaidia watu hao, wanaokabiliwa na changamoto nyingi.
Kambi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa sasa ina zaidi ya Wazee 100, kwa muda mrefu sasa watu hao wamekuwa ni omba omba katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza.
Vitu hivi endapo kama havita chuchukuliwa hatua na kuwasaidia yanaweza kuwasababishia magonjwa mbalimbali, sasa nilazima wadau wengine wajitokeze kusaidia kambi hizi, alisema mama Magufuli.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli (wa pili kulia) akikabidhiwa sehemu ya misaada mbalimbali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, kwa ajili ya kusaidia kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mke wa Rais Dk. John Magufuli, Janet Magufuli, akiwahutubia wananchi wakati wa hafla ya kukabidhi misaada kwenye kambi ya Wazee ya Bukumbi iliyopo Wilaya ya Misungwi, Jijini Mwanza.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...