Leo Ijumaa Kuu Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela amezindua mafunzo ya watoto yanayo endeshwa na shirika la Compassion International (shirika la Shirika ka Kikistro  ambalo lipo nchi 28 duniani, Shirika hili linahudumia zaidi ya watoto 4000 wa madhehebu yote mkoani Iringa. Mafunzo yatolewayo ni pamoja na;
1. Ulinzi wa Mtoto
2.Taarifa sahihi kuhusu VVU na UKIMWI
3.Ukombozi wa kiroho
4.Urafiki na urafiki wa siri
5.Ujasiliamali
6. Kulea maono 
7.Stadi za Maisha
8. haki na wajibu wa Mtoto
9. Huduma na msaada wa Kisaikolojia
10. Kupambana na unyanyasaji na ukatili wa watoto.

Mhe Kasesela ametoa  rai kwa wazazi kushiriki katika masomo na kulea vipaji vya watoto, na amewashauri waunde vikundi ambavyo vitawafundisha uongozi na ujasiliamali, ambapo kila kikundi kintakiwa kiwe na watoto 20. Pia amewaambia waandae wazo ambapo kikundi chenye wazo zuri kitapata zawadi ya shilingi laki 1. Vikundi 5 vyenye mawazo mazuri vitachaguliwa. Pia ameahidi kuhakikisha watoto wanalindwa. 
"Ilikuwa siku nzuri sana kweli namshukuru MUNGU...", Mkuu huyo wa wilaya aliiambia Globu ya Jamii.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akizindua mafunzo ya watoto yanayo endeshwa na shirika la Compassion International shirika la Kikristo  ambalo lipo katika  nchi 28 duniani.
  Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akishiriki mafunzo ya watoto yanayoendeshwa na shirika la Compassion International
 Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya  watoto yanayoendeshwa na shirika la Compassion International
 Irene Lyandala akisoma risala ya washiriki ya mafunzo hayo
Sehemu ya watoto wanaohudhuria mafunzo hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...