Mtu mmoja mkazi wa Mbangala – Chapwa wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina la Erasto Vickson [17] alifariki Dunia baada ya gari yenye namba za usajili T.806 ABY aina ya mitsubishi Fuso lori lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Masoud Wilson Nzowa kushindwa kupanda mlima na kisha kurudi nyuma.

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 15.03.2016 majira ya saa 09:45 asubuhi huko mtaa wa Chapwa, kata na tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya. 

Inadaiwa kuwa, marehemu ambaye alikuwa abiria kwenye gari hilo aliruka toka ndani ya gari baada ya kuona gari limeshindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kituo cha afya Tunduma. Dereva alikimbia baada ya tukio. Upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi  anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria. 

Imesainiwa na:
[Ahmed Z. Msangi – SACP]
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...