![]() |
Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya kwa sasa wameacha nazo katika Iringa Sober House |
![]() |
Mlezi wa kituo hicho cha Iringa Sober House Bw. Godwin Msillu (kushoto) akiwa na baadhi ya vijana waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya ambao wanaishi kituoni hapo |
![]() |
Shadrack John ambae ni mdu anaeishi katika kituo cha Iringa Sober House aliyetoka mkoa wa Arusha akijisomea Biblia baada ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya |
Na Francis Godwin, Iringa
KAMANDA wa umoja wa
vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Bw Salim Asas
ameunga mkono kwa vitendo mapambano ya vita dhidi ya madawa ya
kulevya nchini yaliyoanzishwa na Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kwa kusaidia
uanzishwaji wa kituo cha kusaidia waathirika wa madawa ya
kulevya mkoani hapa.
Bw. Asas ambaye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu alipata kuweka
bayana mkakati wake wa kusaidia vijana walioathiriwa na matumizi ya
madawa ya kulevya ameungana na kituo cha Iringa Sober House
kilichopo Semtema katika Manispaa ya Iringa kuwasaidia vijana hao
ambao afya zao zimeathiriwa na madawa ya kulevya kwa kuwakusanya na
kuwapatia tiba.
Akizungumza
na mtandao wa matukiodaima leo Dr Alli Ngalla ambae ni
Mkurugenzi wa NGOs ya Foundation for Elleviation of drug Addiction andsufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa waathirika
wa madawa ya kulevya cha Iringa Sober House ambacho kimeanza
kufanya kazi chini ya ufadhili mkubwa wa Bw Asas.
Alisema
kuwa kituo kituo hicho toka kimefunguliwa kina zaidi ya mwezi
mmoja ambapo jumla ya wategemezi 7 ambao wanahudumiwa katika kituo
hicho pamoja na wasimamizi watatu ambao pia walikuwa ni watumiaji
wa dawa za kulevya ambao kwa sasa waliacha.
"
Kwa kweli kuendelea kwa kituo hiki kumechangiwa kwa karibu na
Salim Asas ambae amekuwa bega kwa bega kuona vijana walioathirika na
madawa ya kulevya wanasaidiwa na anachofanya salim pia ni kumuunga
mkono Rais Dr Magufuli ambae ametangaza vita dhidi ya madawa ya
kulevya ......hivyo bado tunaomba wadau wengine kujitokeza
kusaidia mapambano haya ya kunusuru afya za vijana wetu "alisema Dr
Ngalla.
Kuwa
lengo la kituo kuweza kuwahudumia waathirika wa madawa ya
kulevya kutoka mikoa mbali mbali nchini hasa wamelenga kuwafikia
vijana wa mkoa wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo tafiti
zinaonyesha mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa matumizi ya madawa ya
kulevya.
Msimamizi
wa kituo hicho Bw Godwin Msillu alisema kuwa mkakati wa
kuanzisha kituo hicho ulitokana na mkakati wa NGOS ya FADAS
ambao walikuja na mpango wa kuanzisha kituo hicho.
Alisema
kuwa kati ya waathirika wa dawa za kulevya ambao wapo kituoni
hapo baadhi yao ni kutoka mkoa wa Arusha na kuwa kumekuwepo na
mafanikio makubwa kwa walengwa hao afya zao kuanza kuimarika na
hivyo kuwataka vijana wengine walioathirika na dawa za kulevya
kutosita kufika kituoni hapo ili kusaidiwa zaidi.
Akizungumza
kwa niaba ya wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw Shadrack
John alisema kuwa amepata kufika mkoani Arusha kuja kupatiwa
huduma hiyo na kuwa kwa sasa hali yake inaendelea vizuri zaidi.
Huku
kijana Ibrahim Abdu alisema kuwa amekuwa akitumia madawa hayo kwa
zaidi ya miaka 10 sasa kabla ya kuamua kuacha na kujiunga na
kituo hicho hivyo kupongeza jitihada za Asas kuunga mkono kituo
hicho huku akiwataka vijana wenzake kuachana na matumizi ya madawa
ya kulevya .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...