Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionyeshwa eneo la uwanja wa ndege itakakopita barabara ya Mchepuko itakayotoka Horohoro kuunga na inayokwenda Pangani kupitia Utofu, Majani Mapana hadi Duga.

SERIKALI ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa kiwango cha lami ambapo mpaka sasa tayari kazi  iliyobaki ni kupata mzabuni wa kuendesha mradi huo.

Waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa ujenzi  wa Barabara hiyo utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 na kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi huo.

Mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja katika  Mto Pangani lenye urefu wa mita 550 ambalo linategemewa kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya kuimarisha shughuli za utalii katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipima eneo la barabara inayohitajika katika eneo la hifadhi ya uwanja wa ndege wa Tanga.

Kwa mujibu wa Prof.Mbarawa ni kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo serikali itawalipa fidia wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa tathimini kwa mujibu wa sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009.

“Nasisitiza kwamba kama sheria inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai kila mwenye haki na anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili hatalipwa na hii itakuwa ni kulingana na tathmini iliyokwishafanyika......”,alisema Waziri huyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama ramani ya gati ya Bandari ya pangani ambayo inajengwa kwa gharama ya sh. bilioni 2.3.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...