Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akiongoza mazungumzo
yaliyomshirikisha Balozi Demnark nchini Bw. Einar Jensen ofisini kwake.
Na Sankana Simkoko – Wizara ya Kilimo
Serikali ya Denmark imedhamiria kupitia wawekezaji kujenga kiwanda cha mbolea hapa nchini
ili kuondoa tatizo la upumgufu wa mbolea kwa wakulima.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Einar Jensen alipomtembelea na
kufanya mazunumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba
ofisini kwake.
“ Tumedhamilia kujenga kiwanda cha mbolea ili kuondoa tatizo la mbolea kwa wakulima wa
hapa nchini Tanzania ” alisisitiza Jensen katika mazungumzo hayo.
Aliongeza kuwa kiwanda hicho kitaweza kuzalisha tani milioni 1.3 kwa kiwango cha chini na
uzalishaji unaweza kuongezeka zaidi ya hapo.
Ujenzi wa kiwanda hiki utawezesha wakulima wa Tanzania kupata mbolea kwa wakati na hivyo
kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali, alifahamisha Balozi Jensen.
Naye Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Nchemba alimfahamisha Balozi Jensen kuwa
Tanzania ina upungufu mkubwa wa mbolea unaoathiri kilimo.
“ Wakulima wamekuwa wakipata mbolea isiyotosheleza mahitaji ya Taifa na pia imekuwa
ikiwafikia kwa kuchelewa sana” alibainisha Mhe. Nchemba
Tanzania ina mahitaji ya mbolea ya UREA, ambayo ni ya kukuzia kwa kiwango cha tani elfu 6 ili
kukidhi mahitaji ya wakulima wetu, Mhe. Nchemba alimweleza Balozi Jensen.
Pia ameitaka Serikali ya Denmark kusaidia kuharakisha ujenzi wa kiwanda hiki ili kuendana na
ilani ya uchaguzi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Mhe. Nchemba alimhakikishia Balozi Jensen kuwa atafanya jitihada binafsi kuhakikisha kuwa
kiwanda hiki kinajengwa haraka iwezekanavyo ili kuinua kilimo hapa nchni.
Kiwanda hicho kinatarajia kujengwa wilayani Kilwa katika mkoa wa Lindi na kwamba tayari eneo
limepatikana kinachofanyika kwa sasa ni kukamilisha taratibu za kisheria.
Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe.
Nchemba na Balozi Jensen kukutana katika harakati zao za kuona sekta ya kilimo, mifugo na
uvuvi vinasaidia kuondoa umasikini kwa Watanzania waliowengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...