Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mh. Halima Dendegu, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shindano la kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na hatimae mchanganuo wa biashara (Statoil Heroes Of Tomorrow BusinessCompetition) lililofanyika Mkoani Mtwara jana.
 
SHINDANO la kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na hatimae mchanganuo wa biashara (Statoil Heroes Of Tomorrow Business Competition) limefanyika Mkoani Mtwara jana, na kufanikiwa kupata majina 10 ya vijana waliofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro hicho.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano hilo,Meneja wa shindano hilo, Erick Mchome alisema, Mashujaa wa kesho (
Heroes of tomorrow) ni shindano linaloendeshwa na kampuni ya Mafuta na gesi kutoka Norway hapa nchini ya Statoil ikiwa na lengo la kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa kutafuta vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 25 ambao watakuwa na mawazo mazuri ya biashara na kuwasaidia katika ndoto zao hizo kwa kuzifanya kuwa kweli.

“Shindono linalenga vijana kutoa mawazo yao ya kibiashara ambayo baadae yatafanywa kuwa biashara” alisema Mchome.

Shindano hilo limeanza na vijana wa Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo vijana 400 walijitokeza kushiriki wakilenga maswala ya kilimo, ufugaji, IT, viwanda vidogodogo na maswala mengine yanayohusiana na biashara ambapo baadhi walijikusanya kama kikundi na wengine mmoja mmoja. 40 bora walichaguliwa kushiriki katika mafunzo ya ujasilia mali yaliyo lenga kukuza na kuendeleza biashara ili ziwe na mafanikio, ambapo katika hilo kumi bora walichanguliwa.
Walio chagulia kumi bora ni Razaki Kaondo, Nyenje Chikambo, Edward Timamu, Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, Sifael Nkiliye, Said Selemani, Yunus Mtopa, Yahay Omari, Kastus Kambona na Abdalah Selega. Hata hivyo mchakato bado unaendelea kwani kumi hawa watachuana vikali kwa kuleta michanganua yao ya biashara ambayo itafanyiwa tathmini na baraza la Jury ili kuwapata tano bora na hatimae mshindi.

“Tano bora watatetea michanganuo yao ya biashara mbele ya baraza la Jury” alisema Mchome ikiwa ni sehemu ya kumtafuta mshindi wa shindano hilo.

Mshindi atapatikana tarehe 15 Aprili jijini Dar es salaam, atazawadiwa dola za kimarekani 5000 wanne walio ingia tano bora kila mmoja wao atajipatia dola 1500 na waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja wao atapata dola 1000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...