Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akizungumza wakati wa siku ya Utepe Mweupe ambapo na uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Pia mama Samia amewasihi wanawake kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya ili kusaidia vituo vya afya. Pia amewataka wananchi kuachana na mila potofu hasa za ukeketaji kwani ni kumkosoa mwenyezi Mwenyezi Mungu.
Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Bakari Kambi akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya Upete Mweupo kwa niaba ya Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, Jinsia, wazeee na watoto, Ummy Mwalimu leo katika uzinduzi wa kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika siku ya Utepe mweupe jijini Dar es Salaam leo na uzinduzi wa mpango mkakati wa kuzuia vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi wa siku ya Utepe Mweupe leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...