Na Shamimu Nyaki - WHUSM.

Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes imekabidhi ipadi 180 kwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kurahisisha utendaji kazi wa Maafisa Habari wa wizara hiyo.Ipad hizo zimekabidhiwa leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Startimes Bw.Lanfang Liao ambaye amehaidi kutoa misaada ya vitendea kazi zaidi kwa wizara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya habari.

“Kampuni yetu na Wizara ya habari zina ushirikiano wa muda mrefu hivyo, tumeamua kuwakabidhi ipadi 180 zenye thamani ya shilingi milioni 90 ili ziweze kusaidia Wizara katika kazi zake”alisema Liao.

Bw Liao ameongeza kuwa, wataendelea kuongeza chaneli nyingi za Kiswahili zitakazokuwa na maudhui yatakayojikita katika nyanja za utamaduni na Sanaa za kitanzania.Naye Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mbali na kuishukuru kampuni hiyo amesema kuwa Ipadi zitagaiwa kwa mikoa 15 ambayo maafisa wake wana uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.

“Ni faraja kwamba wenzetu wa Startimes wametuelewa haraka na kukubali kutusaidia vifaa hivi vya mawasiliano (Ipadi) ,kwa hakika vitatusaidia sana kuboresha utendaji kwa maafisa wetu wa Wizara pia Maafisa Mawasiliano ambao ni wadau wa kutoa taarifa kwa Umma”alisema Nnauye.

Mhe.Nnauye ameongeza kuwa,Wizara ya habari ina lengo la kuimarisha mawasiliano Serikalini kwa kuhakikisha maafisa habari ambao wanafanya kazi kwenye Halmashauri zote kupata vitendea kazi kwahiyo anatoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuboresha mawasiliano kwa Sekta ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Hivyo basi maafisa habari wanapaswa kuzitumia Ipadi hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta maendeleo katika sekta ya habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel (kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akifurahia kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa, Elisante Ole Gabriel na wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na muwakilishi kutoka ubalozini Bw. Mr Gao Wei. 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiteta jambo baada ya kupokea Mini Pads 180 kutoka kampuni ya StarTimes kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Pamoja naye kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dr. Lu Youqing.Picha na Dotto Mwaibale.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...