Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa mshtuko taarifa za kuwepo makundi ya watu na makampuni wanaochezesha michezo ya kubahatisha inayohusu mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na kusimamiwa na TFF (betting).

TFF inauthibitishia umma wa watanzania kuwa Shirikisho halihusiki wala halijawahi kutoa kibali chochote cha kuhusisha mashindano yake na michezo ya kubahatisha.

Kwa kuwa baadhi ya wahusika wa matendo hayo ni makampuni ya nje ya nchi hivyo TFF imechukua hatua zifuatazo:

1.TFF imeandika barua kwenye Shirika la Bahati Nasibu ya Taifa ili kupata mwongozo wa kisera na kisheria kuhusu haki na majukumu ya Shirika hilo  katika kudhibiti na kusimamia  jambo hilo.

2.TFF imeandika barua kwa kitengo cha sheria cha FIFA ili kupata mwongozo na ushauri wa namna ya kudhibiti makampuni ya nje yanayoshiriki mchezo huu.

TFF inawaomba wadau wa mpira wa miguu na washiriki wa michezo ya kubahatisha wajiepushe kushiriki michezo ya kubahatisha inayohushu michezo yote inayoandaliwa na TFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Muongozo wa nini tena wakati ninyi ndo mmpewa jukumu la kuongoza!! TFF hebu nipeni muongozo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...